playlist_add

BANGOKWELI.COM

BILA WEWE KUJULIKANA!
Andika ujumbe na ufahamishe umma au taasisi na vyombo vya usalama.

Una kila sababu sasa!

Shiriki kuhamasisha maendeleo na ustawi wa jamii inayokuzunguka na taifa kwa ujumla. Toa ujumbe kuashiria kero zinazoikumba jamii hususani katika nyanja za Afya, Mazingira, Usalama, Uhamiaji, na kero mbalimbali bila wewe kujulikana. Ujumbe wako utadhibitishwa na kuchapishwa kwa uma punde tu baada ya wewe kuuwasilisha.

Kwa nini BangoKweli?

Watu wengi wanafahamu masuala mbalimabli yanye kuhitaji kupewa vipaumbele hususani taarifa zinazohusu usalama, lakini kutokana na udhalimu, wengi hukwepa jukumu la kutoa taarifa hizo kwa kuhofia kutambuliwa kuwa ni wao ndio waliotoa taarifa hizo. Asante kwa TEHAMA, leo utaweza kutoa taarifa hapa kwa mtindo wa Bango!, na ukabaki na amani bila kujulikana kabisa.

Jinsi ya Kushiriki.

Bonyeza alama ya Andika Bango, au bonyeza kitufe cha mviringo kilicho chini kulia kwa kifaa chako. Tutapokea ujumbe wako na kuupitia kisha kuuchapisha punde tu baada ya kuwasilisha. Pia waweza kusoma mabango yaliyowasilishwa na wazalendo wengine bonyeza Tazama Mabango.

Hamasisha kwa kupigia kura bango kusisitiza ukweli wake na kupelekea mfumo wetu wa BangoKweli! kutuma ujumbe huo moja kwa moja kwa vyombo husika kutegemea na kategoria ya bango hilo.

Ahadi yetu.

BangoKweli! imehamasishwa na dhana ya uhuru wa kutoa taarifa bila kufahamika kutokana na uzito wa ujumbe huo. Hivyo hatutaki na hatuna sababu ya kuchukua taarifa za kuhusu mleta bango. Lengo letu ni kuweka jukwaa huru lisilohitaji usajili wa kumjua aliyetoa ujumbe ni nani na wala alitumia kifaa gani.

Tahadhari!

Sio kila bango utakalo andika hapa litachapishwa, hivyo ni matumaini yetu kuwa utatumia jukwaa hili kutoa bango lenye ukweli na lenye mtazamo chanya kwa maslahi ya jamii inayokuzunguka na taifa kwa ujumla. Hatutaruhusu lugha chafu au ujumbe wenye kuashiria uchochezi ama udhalilishaji wa namna yoyote ile. Kila bango litapitiwa na wahariri wetu kabla ya kuchapishwa, endapo halitakidhi vigezo, bango hilo litafutwa bila kusita.

Karibu sana. Tazama Mabango